Filamu hii inaeleza jinsi ambavyo mwathiriwa aliyedhulumiwa kingono, anaweza kupatiana au kutopatiana ruhusa ya kuendelea na tathmini ya matibabu kabla ya, wakati ama baada ya uchunguzi wa matibabu. Filamu hii inafaa kutazamwa na mwathiriwa.
Filamu yenyewe imetengenezwa na shirika la Physicians For Human Rights kupitia Programu yao inayo uhusika na dhuluma wa kingono katika eneo za vita na machachari, na inalenga kuimarisha mafunzo ambayo Programu hii hupangia wataalamu wa: kidaktari, utekelezaji wa sheria na kisheria kuwasaidia kukusanya na kuhifadhi ushahidi wa dhuluma wa kingono.